Advertisements

Monday, October 24, 2016

2ND FREE QUICKBOOKS TRAINING2ND FREE
QUICKBOOKS TRAINING
Date: October 29, 2016
Time: 2pm to 5pm. 
Venue: 
4600 Powder Mill Rd Suite 450 
Beltsville, MD 20705


Limited Space Available
or
Call: 301-613-5165
Kichupa cha leo Jerry Julian - Welcome Home To Africa (Official HD Video)

SERUWAGE CONSULTING AND CPAs
Seruwage Consulting and CPAs specializing in providing quality services which include:-


1.                  Affordable Life insurance packages
2.                  Funeral Insurance
3.                  Accounting and book keeping for businesses and non profits
4.                  Payroll for Businesses
5.                  Financial auditing, Review and Compilation
6.                  IRS audit help and representation to the IRS
7.                  Medicare Heath insurance
8.                  Starting business help:  registration, licenses , etc
9.                  Business plan

10.            Many other services

 Contact us at info@seruwagecpas.com or 301-613-5165.

KICHUPA CHA LEO NISAMEHE BEXY WAMUSIC OFFICIAL VIDEO directed by shack

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo  ,Ikulu jijini Dar es Salaam


                               .....................................................................
Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi yake itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Balozi huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya Italia na Tanzania.
Amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya kimaendeleo kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na kuimarisha ustawi mzuri katika jamii hapa nchini.

WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.

MTOTO ATEKWA, GARI LAIBWA JIJINI DAR

Mtoto wa miaka mitatu wa askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Kapteni Innocent Dallu ametekwa na watu wasiojulikana baada ya mzazi huyo kumuacha ndani ya gari pamoja na mwenzake ili aingie buchani kununua kitoweo.
Watekaji hao walimshusha mtoto mmoja na kuondoka na mwingine anayejulikana kwa jina la Light.
Kapteni Dallu ni ofisa afya wa JWTZ ambaye alikuwa akifanya kazi Hospitali ya Lugalo, lakini kwa sasa amehamishiwa Darfur nchini Sudan. Kwa sasa yuko jijini Dar es Salaam kwa mapumziko.
Kapteni Dallu amesema tukio hilo lilitokea jana saa 6:00 mchana eneo la Mbezi Juu wilayani Kinondoni baada ya kuhudhuria ibada katika Kanisa la Roma Mbezi Juu.
Kapteni Dallu amesema mtoto huyo ana rangi ya maji ya kunde, mwembamba na alikuwa amevaa gauni la rangi ya bluu.

MAKAMBA ASIKITISHWA NA UPUNGUFU WA MAJI KATIKA ZIWA RUKWA, ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI

Na Lulu Mussa, Sumbawanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.

Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.

“Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.

Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru Ziwa Rukwa.

SARE ZA CCM ZAMSHUSHA CHEO MWALIMU MKUU

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM kwenye mahafali ya kidato cha nne.

Pia, taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta michango yote mashuleni.

Otieno, ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.

MAGAZETI YA LEO OCTOBER 24, 2016

MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

 Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.
 Mfalme wa Morocco Mohammed VI  akipokea shada la maua alipowasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya  kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.

Sunday, October 23, 2016

SHINDANO LA DANCE 255

Angalia video mbalimbali za Shindano la Dance 255 kupitia Vijimambo Blog. Waandishi wa Vijimambo Blog watakuwepo masaa yote eneo la Jamhuri Stadium Kuhakikisha haupitwi na jambo lolote linalihusu Dance 255.

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv DANCE 255

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv

Millennium Tv

Team nzima ya Millennium Stars Entertainment iko bega kwa bega na Crew nzima ya Vijimambo Radio na Vijimambo Blog kuhakikisha haupitwi na habari yoyote kuhusu Shindano la Dance 255. Hii itakua Exclusive Show kupitia Simu yako ama Komputa yako. Ni rahisi sana, Subscribe kwenye YouTube Chanel ya Millennium Tv uzidi kuwa karibu na Ulimwengu wa Burudani siku zote.

DANCE 255 KUANZA KUTIMUA VUMBI OCTOBER 29 UWANJA WA JAMHURI DODOMA

PATA TASWIRI YA AROBAINI YA MRS ZERAH CHIMPHAYE BANYIKWA


Arobaini Mrs Zerah Chimphaye Banyikwa  mama yake na Mary Ngola iliyofanyika katika Holy Trinity Lutheran Church, Mulberry  St, Yorkers New York. 


 Mchungaji akiongoza misa kanisani hapo 
 Mary akiwa na mume wako na mtoto wao kanisani hapo. Kwa  picha zaidi nenda soma zaidi.

ENDELEA KUPATA UPDATES ZA SHINDANO LA DA NCE 255 KUPITIA VIJIMAMBO BLOG

Shindano la kusaka Vipaji vya dancers linalojulikana kama Dance 255 linatarajiwa kuzinduliwa rasmi mnamo tarehe 29, October 2016 katika Viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma. Team nzima ya Vijimambo Radio na Vijimambo Blog itatia kambi katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma kipindi chote cha Mahindano kuhakikisha haupitwi na taarifa juu ya jambo lolote.

Angalia Baadhi ya Vipaji vilivyoonyeshwa katika kipindi cha Usaili uliokua ukiendelea katika Viwannja Vya Nyerere Square Mkoani Dodoma. Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment na Muandaaji wa Shindano hili ndg. Josias Charles ameahidi kuhakikisha taarifa zote unazipata kupitia Vijimambo Blog.


 Usaili wa Dance 255 Dodoma Viwanja Vya Nyerere Square.
https://youtu.be/nxQF4zk8Ueo

RATIBA YA MAZISHI YA JACOB ELINAZA

Ratiba ya mazishi Jacob Elinaza yatakayo fanyika Oktoba 24,2016 nyumbani kwao Segerea jijini Dar es Salaam.

1. Mwili wa marehemu utafika saa 11:30 am 
2. Chakula cha mchana kuanzia 12:00pm 
3. Kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 2:30pm 
4. Ibada ya mazishi itaanza kuanzia 4:00pm 
Kila kitu kitakuwa nyumbani kwetu segerea kwa mama 
*Maelekezo* ya kufika

Unashuka kituo  cha Oil com segerea anachukua pikipiki unasema wakupeleke kwa msoji mwanajeshi au kwenye msiba kwa Elinaza 
    
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Accounting and Bookkeeper (Non Paid Internship, Start ASAP)We are looking for an Accounting Student/Accountant/Bookkeeper, 


who will maintain records of financial transactions by QuickBooks, learn tax preparation and learn about other accounting areas.We will Train . The ideal candidates should have relevant knowledge of bookkeeping and accounting principles. Please note this is a Non Paid Internship. 

The responsibilities are likely to include:
 • Record day to day financial transactions and complete the posting process by QuickBooks
 • Verify that transactions are recorded in the correct day book
 • Prepare monthly bank reconciliation
 • Process accounts receivable/payable and provide payroll data with CPA in a timely manner
What to expect from you:
 • A College student is generally required, BSc/BA diploma in business or relevant field is a plus
 • To be able to work for at least 8 hrs a week
 • Solid understanding of basic bookkeeping and accounting payable/receivable principles
 • Hand-on experience with spreadsheets 
 • Proficient in MS Office
 • Must have outstanding interpersonal and communication skills
 • Be detail-oriented with high degree of accuracy
 • Proven experience as accounting or similar positions is a plus

How to Apply:
*Please send your resume and cover letter to iddi@seruwagecpas.com


Thank you.

UPDATE YA ERIC MAGAMBO FUNDRAISING

Eric Magambo na mmwanae

Gofundme jumla makusanyo yaliyokusanywa $3,125/= ukitoa makato ya gofundme $261.79 tumebaki na $2,863.21 wanajumuiya Houston makusanyo yao ni $2,066/= fedha ya BOA ni $823/= jumla ya makusanyo yote ni $5,752.21/= lengo la makusanyo ni $5,000/= tumezidisha makusanyo kwa $752.21/=.

Kama tulivyosema hapo awali
Familia ya Magambo na Eric mwenyewe wakiwemo ndugu na marafiki wa Eric walioendesha zoezi zima la ukusanyaji michango wa Eric Kwa ajili ya mwanasheria wa uhamiaji wanashukuru mno kwa wale wote walioguswa na kujitoa mhanga na kuchangia kadri walivyoweza na wengine kusaidia kusambaza ujumbe kwa ndugu na marafiki zao ikiwemo mitandao mbali mbali.

Eric Magambo amtokwa na machozi hakuamini hiki kikubwa mlichofanya kwa ajili yake, ameshukuru mno na tutakuwa tunawaarifu kila tutakapofikia

TUNAWASHUKURU MNO

Kwa maelezo zaidi na swali kuhusiana na Eric Magambo wasiliana na

Shaneisa Magambo 412 520 2029
Jabir Mudrika 202 391 9153
Prosper Magambo +255 767 802255
Idd Sandaly 301 613 5165
Dj Luke Joe 301 661 6696
Dany Kiondo 832 507 1297


Asanteni sana kwa msaada wako

Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi

Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania. 
Mmiliki wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria. 
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) akimlisha keki Mmiliki wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria. 

CHAWABATA CHAIOMBA SERIKALI KURUDISHA MUDA WA ZAMANI WA KUFUNGUA BAA NCHINI

Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na  waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.

Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.  akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale


CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.


Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein wakati akizungumza na mtandao wa  www.habarizajamii.com Dar es Salaam leo asubuhi  kuhusu changamoto waliyonao wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na vinywaji baridi.

DC LONGIDO,DANIEL CHONGOLO AMSWEKA NDANI MKANDARASI WA BARABARA

DC-Longido,Mh Chongolo.
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja  na wananchi kwa ujumla. 

Mkandarasi huyo anayemiliki kampuni ya Genuine Company Limited amekuwa akiendesha shughuli za ujenzi wa drift katika barabara hiyo bila kutengeneza barabara mchepuko (diversion) katika maeneo hayo na kusababisha mara kwa mara wasafiri kukwama na kulala porini. 

Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema Mesiaki Laizer.

MANA CONFERENCE 2016 WASHINGTON, DC