Advertisements

Tuesday, August 30, 2016

SERIKALI KUTOA AJIRA MPYA 71,496

Serikali inatarajia kutoa ajira mpya zipatazo 71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaondoa wafanyakazi hewa ambapo hadi sasa watumishi wapatao 839, tayari wapo katika hatua mbalimbali wakiwepoo waliopelekwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,(Utumishi na Utawala Bora),Angela Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia juu ya utekelezaji na mikakati katika Wizara yake katika kipindi cha “Utekelezaji” kinacho rushwa kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC1). 

“Mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi hewa waliofanyiwa mahojiano na polisi na kama upelelezi ukikamilika sheria kali zitachukuliwa ikiwepo kufikishwa mahakani kwa mtumishi atakaye bainika kukutwa na makosa “ Alisema Kairuki 

Alisema kuwa kuna baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu ambao wameonekana kuwa si waaminifu kwani baadhi yao wameonekana kuelekeza fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini majina yao yameonekana bado kuendelea kuwepo katika mfumo wa kupokea. 

Kairuki aliongeza kuwa katika kipindi cha Machi mosi mpaka kufikia Agosti 20 mwaka huu, Watumishi hewa wapatao 16,127 walibainika ambapo walikuwa wakisababishi hasara ya mabilioni kwa serikali ambapo serikali kama ingewalipa ingesababisha hasara ya zaidi ya bilioni 16. 

“Uhakiki huu ni endelevu kwani baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu si waaminifu hivyo tunawataka waajiri wao kuweka mkazo katika swala hili, kwani tunajua wahasibu wengi wamepewa madaraka lakini si waamiifu”Alisema Kiruki. 

Kairuki aliwatoa hofu baadhi ya Watanzani ambao walikuwa wakisubiria ajira mpya kutoka Serikali, alisema kuwa kilichokuwa kikisubiriwa ni takwimu halisi ambazo zitasaidia kuonesha ni watumishi wangapi wameweza kuondolewa. 

“hii ni neema kwa wanafunzi waliomaliza vyuo kwani kuna nafasi zipatazo 71,496 kwa mwaka huu wa fedha hivyo napenda kuwahauri vijana kuwa na subira kwa kuto kujiingiza katika makundi yasiyo faa” Alisema kairuki. 

Pia aliwataka Maofisa Utumishi kuwa hudumia vizuri watumishi kwa kuwapa haki zao ikiwemo kuwa pandisha madaraja kwa wakati stahili na si vema kwa baadhi ya watu kughushi taarifa za Utumishi wa umma na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni kosa kuibwa sana. 

No comments: