Advertisements

Wednesday, September 28, 2016

OMAN YAONESHA NIA YA KUKARABATI JENGO MAARUFU LA 'HOUSE OF WONDERS'-ZANZIBAR

.Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sultanate of Oman, Dkt Augustine Mahiga ( kushoto) na Yusuf bin Alawi bin Abdullah wakizungumzia kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo hayo Waziri Mahiga ameiomba serikali ya Oman kupitia Waziri Abdullah kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika uhifadhi ya nyaraka na kumbukumbu muhimu pamoja na ukarabati ya jengo la House of Wonders lilojengwa na ufalma wa Oman mwaka 1883
Jengo maarufu la Beit Al Jaib ( House of Wonders) ambalo Serikali ya Tanzania inaiomba Serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa kulikarabati kama sehemu ya mradi wa kuhifadhi nyaraka, kumbukumbu na majengoa ya kihistoria visiwani Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika, Mazungumzo yao yalijielekeza zaidi katika uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Na Mwandishi Maalum, New York

Ufalme wa Oman umeonesha nia ya kukarabati majengo ya makubusho ya kale ya Beit Al Jaib maarufu kama “ House of Wonders” yaliyopo mjini Unguja – Zanzibar.

Nia hiyo imeoneshwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Addullah wakati alipokutana na kufanya mazugumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga.

Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yalifanyika pembezoni mwa Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo Mawaziri hao walikuwa wakiongoza ujumbe wa Nchi zao.

Mazungumzo ya Mawaziri hao yalijikita katika uimarishwaji wa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Oman na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika majadilaino hayo ambapo pamoja na mambo mengine, Waziri Mahinga aliomba serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa kuanzishwa kwa miradi wa kutunza mambo ya kale zikiwamo nyaraka muhimu zinazohusu uhusiano baina ya nchi hizo mbili

Waziri Mahiga alieelezea pia hali uchakavu wa majengo ya Beit Al Jaib ( House of wonders) majengo yaliyokuwa Ikulu ya utawala wa Kifalme, Zanzibar. Makubusho hayo yamesheheni historia ya uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na Sultanate of Oman na Afrika Mashariki kwa Ujumla.

Na kutokana na historia hiyo na umuhimu wa jengo hilo ambalo limejengwa mwaka 1883, Waziri ameiomba Serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa kulihifadhi jingo hilo ambalo pia ni kivutio kikubwa cha utalii.

Akijibu ombi hilo na mengine yaliyowasilishwa na Waziri Mahinga, Waziria wa Mambo ya Nje wa Oman, Bw . Yusuf bin Alawi bin Addullah amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuandaa andiko na kuliwasilisha katika Serikali ya Oman ili pendekezo hilo liweze kufanyiwa kazi pamoja na mapendekezo mengine.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga amekuwa na kuwa na mazungumgo na Bi. Linda Thomas Greenfield, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika.

Mazungumzo ya Waziri Mahinga na Bi. Linda Greenfield yalijikita zaidi katika uhusiano na ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani.

1 comment:

Anonymous said...

Huku kuomba kwingine ni fedheha sana....nchi mnaingiza mamilioni ya dolla mnashindwa kukarabati jengo hili mnaenda kuomba????...hivi sisi nani katuloga?