Advertisements

Wednesday, February 22, 2017

WAZIRI MAKAMBA AWATAKA WACHIMBAJI MCHANGA NA WALIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA KUONDOKA MARA MOJA KATIKA BONDE LA MTO MSIMBAZI HUKO VINGUNGUTI .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo. Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.

Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.

Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo.

(habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mtop Msimbazi katika kata ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti kukagua athari mbalimbali za mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi.

No comments: